Kombora la Korea kaskazini
Maafisa wa kijeshi nchini Korea Kusini wanasema Korea Kaskazini imejaribu kurusha kombora kutoka kwa manowari ya kivita na kukiuka vikwazo vya kimataifa
Wanasema kuwa kombora hilo hatahivyo lilifeli muda mfupi baada ya kurushwa
Urushaji huo wa kombora unajiri baada ya Korea Kusini na Marekani kukubaliana kuweka mitambo ya kujikinga dhidi ya makombora nchini Korea Kusini. Rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un na maafisa wake wa kijeshi
Mitambo hiyo ina uwezo wa kutambua makombora na kisha kuyadungua.
Nchi hizo mbili ziliafikia mpango huo baada ya majaribio kadha ya makombora yaliyofanywa na Korea Kaskazini mapema mwaka huu.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)