Kapteni wa JWTZ Apanda Kortini Kwa Kutishia Kuua


KAPTENI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Tanzania (JWTZ), Henrick Mahenge (34) mkazi wa Mliman City, Dar es Salaam, juzi alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashitaka ya kujaribu kumuua askari wa usalama barabarani.


Akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan, Wakili wa Serikali, Grace Mwanga alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai 12, mwaka huu maeneo ya Mnazi Mmoja wilayani Ilala. Mwanga alidai kuwa mshitakiwa alijaribu kumuua askari wa usalama barabarani WP 5177 Clesensia Makanyaga.


Mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo.


Hata hivyo, Mwanga alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na kwamba hali ya mgonjwa haijulikani hivyo aliomba mahakama izuie dhamana hadi watakapopata uhakika kuhusu hali ya mgonjwa.


Mshitakiwa alipopewa nafasi ya kuelezea kilichotokea, alidai hakutishia kuua na kwamba yeye ndiye alifanyiwa fujo na kuchaniwa nguo zake na kwamba alimuona mshitakiwa baada ya tukio na kwamba hakupata taarifa kuwa mlalamikaji yupo hospitali.


Hakimu Hassan alisema kuwa dhamana ipo wazi kwa wadhamini wawili kutoka taasisi zinazotambulika na kuwataka wakaguliwe kwanza kujiridhisha.


Alisema pia mshitakiwa arudishwa rumande hadi Julai 19 mwaka huu watakapojiridhisha na wadhamini pamoja na kujua hali ya mlalamikaji.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top