Chadema:Maandamano yako pale pale Septemba Mosi


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesisitiza kuendelea na dhamira yake ya kufanya maandamano nchi nzima ifikapo Septemba Mosi, mwaka huu licha ya Rais John Magufuli kutoa tahadhari dhidi ya kitendo hicho leo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Singida.


Hayo yamesemwa usiku huu na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji katika kipindi cha Mada Moto kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Channel Ten jijini Dar es Salaam.


“Lengo letu tunataka kuwaeleza wananchi hasa wanachama wa chama chetu maazimio tuliyokubaliana katika mkutano wetu uliomalizika hivi karibuni,” amesema Dk Mashinji.


Amesema Chadema hawakusudii kufanya vurugu bali watafanya maandamano ya amani yanayolenga kwenda kupokea taarifa ya mkutano.


“Nashangaa ni kwanini maandamano haya yanawatia hofu watawala kiasi cha kutaka kuyazuia na wala hatuhitaji ulinzi wa polisi, tutaenda kwa amani tu,” amesema katibu mkuu huyo.


Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top