BAADHI YA MASHABIKI WA SIMBA WAMKATAA DEWJI


Baadhi ya mashabiki wa timu ya Simba wamepingana na hatua ambazo zinataka kuchukuliwa na Bilionea kijana, Mohammed Dewji juu ya mpango wake wa kutaka kununua hisa za asilimia 51 kwenye klabu hiyo



Mmoja wa mashabiki hao aliyejitambulisha kama Mgeni Ramadhani jina maarufu dogo Macho amesema kwamba,Mohamed Dewji hastahili kupewa timu ya Simba kabisa awali alipokua anaidhamini timu hiyo alishindwa kuiendesha timu hiyo kwa weledi na kupelekea kuikimbia Simba wakati Simba inacheza ligi ndogo mkoani Morogoro


Amesema kwamba Dewji alishindwa kutimiza maagizo yake ambayo aliyatoa kwa wanachama ikiwa ni pamoja na swala lake la kujenga uwanja na vitega uchumi kwa maendeleo ya Simba


Hata hivyo amewatahadharisha wanachama hai wa Simba kuelekea kwenye mkutano mkuu na kuwa  makini na jambo hilo kwani wasipokua makini linaweza kuleta athari kubwa kwa timu hiyo hapo mbeleni


Nae mshabiki mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Tifa Ramadhani Simba,amesema kwamba kwa upande wake nae pia anapingana na matakwa ya Mohamed Dewji juu ya kutaka kununua hisa za asilimia 51 ndani ya klabu hiyo kwani hakuna utaratibu mzuri ambao umetumika kwa ajili ya kumpata mwekezaji sahihi.
 

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top