Zitto Kabwe ajitokeza na kuongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya ACT-Wazalendo, hivi ndivyo alivyosema



Mh: Zitto Kabwe akiongea na waandishi wa habari muda mfupi makao makuu ya chama cha ACT WAZALENDO 
Pamoja na mambo mengine amelituhumu jeshi la polisi kwa
kitendo cha kumvizia wakitaka kumkamta,
anasema hajui ni kwanini Polisi wamezuia Kongamano lao la Kuchambua Bajeti.

''juzi usiku siku ya jumaamosi, watu wetu wa usalama wa chama walinijulisha kwamba Jeshi la Polisi wananitafuta, wakaenda nyumbani kwangu na magari manne kunikamata bila kufuata utaratibu''alisema Zitto, na kuongeza kuwa  ''Jumanne iliyopita Kamishna Wambura alinipigia kuniomba nifike polisi''

 ''Hii ya Jumaamosi walikuwa wanataka Kunivizia'' Zitto

.
 ''Watu wetu wa Usalama wa Chama walihakikisha kwamba sitakamatwa ili niweze leo kupata fursa kuzungumza na watanzania kupitia nyie wana habari'  Zitto

 '' Hatufahamu Watawala wanaogopa nini mpaka kuzuia mikutano ya wanasiasa''Zitto

 '' Nasikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Mbowe wa Chadema Huko Mwanza kisa eti kawasalimia wananchi, huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa kidemokrasia''


Zitto ''Tunalaani tabia za KIDIKTETA za Rais Magufuli'' Zitto

 ''Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonyesha Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari, Tumkatalie'' alisema Zitto



 ''Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza alifanya RWANDA, tumegundua kuwa alikwenda kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na Kuongoza Kidikteta'' alisema Zitto

 '' Hauwezi kupamnana na UFISADI kama haumpi nguvu ya Kiutendaji wa CAG'' alisema Zitto


 ''Kwa hali Hii anayokwenda MAGUFULI AJIANDAE KUWA RAIS WA TERM MOJA kwa sababu watanzania hawataweza kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa na Rais DIKTETA KAMA YEYE'' alisema Zitto

 '' CCM wamdhibiti MAGUFULI, na wasipomdhibiti sisi na Watanzania Tutamdhibiti'' alisema Zitto

 '' Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga, akimfunga Zitto watazaliwa wakina Zitto wengine, na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama kidete mpaka nchi irudi kwenye misingi'' alisema Zitto


 ''IGP ameagizwa na MAGUFULI anikamate, lakini hawezi kunikamata bila kufuata utaratibu, hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi hatukamatwi kwa kuviwa viziwa, tumewaonyesha kwamba Polisi wanaweza klutukamata kwa kufuata terms zetu na sio zao'' alisema Zitto


 '' Karibuni kesho saa tisa kwenye Kongamano letu, Hatuwezi kuacha kufanya siasa, lazima tuendelee kufanya siasa, mmeudhuria mikutano yetu hamjaona hata sisimizi amekanyagwa'' alisema Zitto


 '' Wanasema Bajeti imeongezeka kwa 32% ukweli ni kwamba Bajeti imeshuka kwa maana Dola imeporomoka'' alisema Zitto



 ''CCM wamdhibiti mwanachama wao MAGUFULI, wasipomdhibiti sisi Tutamdhibiti'' alisema Zitto


Jambo leo
Naomba unikumbushe sheria inayoruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano na makongamano

ZITTO ''Sheria ya Vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 inaruhusu vyama vya siasa kufanya siasa, makongamano na mikutano ni sehemu ya siasa, hatuhitaji kuomba kibali

SWALI
Je mkutano utarushwa Live

Zitto ''Tutaweka Utaratibu ili watanzania wengi zaidi waweze kushiriki kwenya kongamano''

 ''Polisi hawana mamlaka ya kisheria Kuzuia Mikutano ya vyama vya siasa, tunaipongeza Chadema kufungua kesi ya kikatiba mwanza, sisi tunafungua hapa Dar, na tunavitaka vyama vingine vifungue kesi ili ziwe nyingizaidi kudai haki'' alisema Zitto


''Kama serikali haifanyi sawa sawa ni wajibu wetu kuwakosoa, na tutawakosoa tutawakosoa kama tulivyokuwa tukifanya serikali iliyopota...serikali ya sasa haina uvumilivu'' alisema Zitto


 ''Bunge limenisimamisha Ubunge, tutatumia Forums nyingine kuwatetea wananchi na Demokrasia...Hatuhitaji kibali cha mtu yeyote kufanya kongamano'' alisema Zitto
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top