Jengo lililoshambuliwa na Al Shabaab
Watu kumi wameuawa katika shambulio la kigaidi mjini Mogadishu nchini Somalia,baada
ya kundi la wapiganaji kuvamia hoteli ya Ambassador na kisha kugonga geti la hoteli hiyo kwa gari lenye vilipuzi. Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa kati ya watu hao kumi waliouawa wawili ni wabunge waliokuwa wakiishi katika hoteli hiyo.

Kundi la Al Shabaab limekiri kutekeleza shambulizi hilo,ikiwa ni saa chache tangu kuuawa kwa kiongozi wao, Mohamed Kuno, Kusini mwa Somalia na ambaye anadaiwa kuratibu shambulizi la chuo kikuu cha Garissa miaka miwili iliyopita.
Hata hivyo haijafahamika mara moja kama wapiganaji hao wamewateka baadhi ya watu katika shambulio hilo.

Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)