Polisi nchini Burundi wanashikilia kundi kubwa la wanafunzi wa sekondari kwa kosa la kuharibu picha ya rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza.
Vijana hao wanakabiliwa na kosa la kumtukana kiongozi wa nchi, kosa ambalo adhabu yake ni kifungo cha miaka mpaka kumi jela.
Wakazi mjini Bujumbura wanasema, watu wawili wamejeruhiwa mwishoni mwa wiki wakati polisi walipopiga risasi kutawanya wanafunzi waliokuwa wakiandamana na kusababisha vurugu.
Kwa mujibu wa habai mwezi uliopita, zaidi ya wanafunzi mia tatu walifukuzwa shule katika mji wa Ruziba baada ya walimu kukuta vitabu vyenye picha ya rais vimeharibiwa vibaya na wanafunzi hao