Wakala wa kudhibiti matumizi ya kusisimua misuli michezoni Wada wameiondoa katika orodha ya maabara zake, Maabara ya kuchunguza utumiaji
wa dawa za kusisimua misuli ya Madrid kwa madai kuwa haina viwango vya kimataifa.
wa dawa za kusisimua misuli ya Madrid kwa madai kuwa haina viwango vya kimataifa.
Zuio hilo linaanza kazi mara moja ambapo maabara hiyo ya Hispania haitaruhusiwa kufanya shughuli zozote za kimaabara zinazowahusu wanamichezo.
Hata hivyo Wada imesema kituo kilichoko Barcelona kimeendelea kusalia na viwango bora huku kituo cha Madrid kikiwa na siku 21 za kukata rufaa juu ya hatua hiyo ambayo mpaka sasa inafanya maabara zinazotambulika ulimwenguni kusalia 30 tu wakati huo Afrika ikiwa haina hata Maabara moja.