Hatimaye Shirikisho la Soka Tanzania TFF, limekubali yaishe kufuatia mvutano ulijitokeza kwenye mchakato wa uchaguzi wa klabu ya Yanga mgogoro wa Uchaguzi wa Yanga baada ya klabu hiyo kutaka ijisimamie yenyewe na si Kamati ya TFF.
Kwa kile kilichoonekana kama kunyanyua mikono, kwenye kikao kilichofanyika leo kati ya uongozi wa juu wa TFF ukiwa chini Jamal Malinzi na Viongozi wa Yanga wakiongozwa na makamu mwenyekiti wa klabu hiyo Clement Sanga, TFF imeamuru klabu hiyo kupitia kamati yake ya uchaguzi iendeshe zoezi hilo.
Sambamba na sakata hilo, Afisa habari wa TFF amewaambia waandishi wa habari kuwa kikao hicho kimetoa maazimio juu ya wanachama waliosimamiswa kufuatia kuchua fomu za kugombea zilizotolewa na kamati ya uchaguzi ya TFF, hivyo waruhusiwe kuendelea na mchakato wa uchaguzi kama kawaida, maazimio ambayo Uongozi wa Yanga umepokea kwa ajili ya kwenda kuyajadili.