Rais Dkt John Pombe Magufuli afuturisha viongozi mbalimbali

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum wakati akiwasili kwa ajili ya kufuturu pamoja na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Abrahaman Kinana Ikulu kwa ajili ya futari ya pamoja na viongozi mbalimbali wa dini Ikulu jijini Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum wakati akielekea ukumbini kwa ajili ya kujumuika pamoja na viongozi mbalimbali wa dini katika futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi mbalimbali wa Dini mara baada ya kufuturu nao pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam


Kaimu Mufti Sheikh Hamid Masoud Jongo akiomba dua mara baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum

Baadhi ya wazee na viongozi wa madhehebu ya dini wakisalimia na Rais Magufuli
Rais Magufuli akisalimia na wakina Mama aliowakaribisha kwenye futari aliyowaandalia Ikulu.
Mke wa Rais wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli akiwa na kinaMama waliohudhuria futari ya pamoja ya viongozi mbalimbali wa dini iliyoandaliwa na Rais Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam​
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top