Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango anawasilisha bajeti ya serikali kuu pamoja na mambo mengine ametangaza kusudio la serikali kufuta
vibali vya misamaha ya kodi kwa bidhaa zote ambazo wanufaika wakuu walikuwa askari wa majeshi yote ya Tanzania, ''Serikali inapendekeza kufuta misamaha ya kodi kwa bidhaa zote za majeshi yote ya Tanzania'' amesema Dkt Mpango. Ameongeza kusema kuwa baadhi ya watu hasa viongozi wanatumia vibaya msamaha huu kujinufaisha wenyewe na kuikosesha serikali mapato mengi. Waziri Dkt Mpango amesema serikali itaongeza posho kwa watumishi wa majeshi yote ili wanufaike moja kwa moja badala ya kutoa msamaha wa kodi''serikali itatoa posho stahiki nje ya posho za kawaida kwa askari wote, ili kuwawezesha askari wote kukidhi mahitaji yao na kuwabana wajanja wachache wanaojinufaisha na misahama hiyo''amesema Dkt Mpango