MATCH PREVIEW: URENO INAPOCHEZA NA ICELAND

Ureno na Iceland wanakutana leo katika kinyang’anyiro cha Euro 2016, kwenye mchezo kundi F utakaochezwa saa nne kamili usiku kunako dimba la Stade Geoffroy Guichard lililopo manispaa ya Saint-Etienne.

Katika mchezo huu Cristiano Ronaldo anatarajia kuvunja rekodi ya Luis Figo ya kucheza michezo mingi zaidi akiwa na taifa hilo.

Ronaldo ambaye ndiye nahodha wa timu hiyo, mpaka sasa ameshacheza michezo 126, huku akitarajiwa kuwepo katika mchezo wa leo na kufikia rekodi ya Figo ambaye alicheza michezo 127.

Kutokana na kuendelea kuwepo katika kikosi hicho, Ronaldo anatarajia kuweka rekodi mpya kwa kucheza michezo mingi zaidi.

Ronaldo alifunga magoli mawili kati ya 7 wakati Ureno iliposhinda mabao 7-0 dhidi ya Estonia, kwenye mchezo wa kirafiki uliolenga kujiandaa na michano hii. Pia amefunga magoli mengi zaidi (5) wakati wa michezo ya awali ya kufuzu kucheza michuano hii na kuisaidia timu yake kumaliza kileleni mwa kundi I.

Ureno watakuwa na matumaini makubwa kutokana na uwepo wa Quaresma na Ronaldo.

Quaresma amekuwa katika ubora wa hali ya juu hivi karibuni hali inayotoa matumaini makubwa kwa kikosi hicho hasa wakishirikiana vyema na Cristiano Ronaldo.

Katika mchezo dhidi ya Estonia, Quaresma alifunga mara mbili na kutoa pasi mbili za magoli.

Mchezo huu unafananishwa na vita kati ya Daud na Goliath, ambapo Iceland wanafananishwa na Daud na Ureno wanafananishwa na Goliath kutoka na kuingia katika mchezo wa leo kama timu yenye nafasi kubwa ya ushindi.

Lakini licha ya kuwa taifa lisilo na nguvu kubwa katika soka, kocha wa Iceland haoni kama watashindwa kufuzu hatua ya mtoano hata ikitokea leo wamepoteza mchezo.

“Kama tutacheza kama ambavyo huwa tunacheza, nadhani tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri na kufuzu kuelekea hatua ya mtoano, lakini hata tukipoteza si mwisho wa mapambano,”amesema kocha wa Iceland Lars Lagerback.

Lakini kwa kutegemea na matokeo ya mchezo wa leo, tutajua namna gani ya kukabiliana na wapinzani wetu katika mchezo wa pili na wa tatu. Kila mtu anaizungumzia Hungary kama timu ambayo tunaweza kupata pointi kirahisi, lakini Hungary sio timu ya kubeza pia. Muhimu hapa ni kuhakikisha tunapata pointi tatu kwenye kila mchezo.”

Taarifa muhimu kwa kila timu.

Meneja wa Ureno Fernando Santos bado ana mashaka endapo nyota wake mahiri Ricardo Quaresma atacheza ama la! kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya misuli.

Mbali na huyo, wachezaji wako salama wakiwemo kinda mwenye umri wa miaka 18 Renato Sanches pamoja na wachezaji wawili wa Southampton Jose Fonte na Cedric Soares.

Iceland itakuwa ikiongozwa na nahodha wake anayekipga Cardiff City Aron Gunnarsson, akisaidiwa na nyota wa Swansea Gylfi Sigurdsson ambaye alifunga magoli sita wakati wa kufuzu hatua kuelekea michuano hii.

Iceland pia watakuwa na mkongwe wao mwenye miaka 37, ambaye ndiyo mfungaji wao bora wa muda wote Eidur Gudjohnsen bila ya kusahau uwepo wa Johann Berg Gudmundsson anayekipiga Charlton Athletic.

Dondoo muhimu
Ureno wanashiriki michuano kwa mara ya saba
Hatua bora kabisa kwa Ureno kuwahi kufika ni wakati walipomaliza nafasi ya pili nyuma ya Ugiriki baada ya kufungwa bao 1-0 kwenye fainali iliyofanyika mwaka 2004 nchini mwao.
Wakati michuano hii ilipofanyika tena nchini Ufaransa mwaka 1984, Ureno walifanikiwa kufika hatua ya nusu fainali na kutupwa nje na wenyeji kwa kufungwa magoli 3-2 katika muda wa ziada.
Ureno hawajwahi kutolewa katika hatua ya makundi. Walimaliza katika nafasi ya kwanza mara nne kwenye michuano sita iliyopita na mara mbili wakimaliza nafasi ya pili.
Iceland watakuwa wakishiriki kwa mara ya kwanza kwenye michuano hii. Nyingine ni Northern Ireland, Wales, Albania and Slovakia.
Itakuwa ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano mikubwa kwa mataifa baada ya kushindwa kufuzu Kombe la Dunia miaka ya nyuma.

Iceland linakuwa la kwanza kushiriki michuano ya Euro, huku jumla ya wakazi wake wakiwa chini ya milioni moja.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top