Leo tarehe June 24, 2016, Wananchi wa Uingereza wameamua kujiondoa katika Umoja wa Nchi za Ulaya kupitia kura za maoni zilizopigwa jana.
Kila eneo la maisha ya Muingereza litaathirika kutokana na maamuzi haya ya wengi wa Waingereza. Na Upande wa michezo nao hauna usalama.
Uhuru wa kwenda popote (Freedom of Movement) ulikuwa unawapa fursa wanamichezo kutoka ndani ya EU kwenda kufanya biashara/kazi nchini Uingereza bila kuhitaji kibali ambacho raia wengi kutoka nchi ambazo hazipo katika Umoja wa Ulaya wanahitaji ili kufanya kazi nchini humo.
Sheria hii pia ipo sawa na kwenye upande wa soka la Uingereza. Kwa sheria za sasa zinazotoa vigezo vya wachezaji kutoka nje ya EU, inamhitaji mchezaji/wachezaji kucheza kiwango fulani cha mechi za kimataifa na timu za mataifa yao ili kuweza kupata kibali cha kucheza England, sheria hii inawabana wachezaji zaidi ya 100 wanaocheza katika ligi kuu ya England kwa sasa.
Wachezaji kama David De Gea, Dimitri Payet, N’Golo Kante na Anthony Martial, ni miongoni mwa wachezaji ambao hawakuwa na vigezo vinavyotakiwa na sheria wakati wakihamia katika vilabu vyao vya sasa. Wachezaji wa South American kama Diego Costa na Philippe Coutinho wote wangeshindwa kupata kibali cha kufanya kazi UK hata baada ya kupata uraia wa Ulaya kabla ya kuhamia England.
Kabla ya matokeo ya kujitoa kujulikana, mmoja wa mawakala wa soka Jonathan Barnett alisema kujiondoa EU kutapunguza ushindani wa Premier League. “Ni muhimu kwamba ikiwa tunataka kuwa na ligi bora duniani basi itabidi tubaki kwenye EU,” alisema. Na kauli hii ileleta maana zaidi baada ya mwenyekiti wa EPL, Richard Scudamore pamoja na vilabu vyote 20 vya EPL vilipiga kampeni ya kutaka Uingereza ibaki kwenye Umoja wa Ulaya.
Kujiondoa kwa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya kumeketa majadiliano makubwa miongoni mwa wadau wa kila sekta na kwa hakika kwenye upande wa soka kutabadilisha mambo mengi.
“Kitachotokea itabidi mamlaka za michezo itabidi wake chini na kuangalia upya kanuni na sheria na kuamua kuendelea nazo au kubadili kuendana na mabadiliko yaliyopo na mataifa mengine ya ulaya, kwa mfano kutoa upendeleo kwa wafanyakazi kutoka mataifa mengine ya EU, au kuangalia sheria zilipo kama zinajitosheleza au inabidi zitengenezwe mpya kabisa?” Maria Patsalos, mmoja wa wahusika wa masuala ya uhamiaji alisema. “Ni vigumu tena kwa wafanyakazi kutoka mataifa mengine ya ulaya kuwa na uhuru kama uliokuwepo nchini Uingereza.”
Changamoto nyingine ambayo itajitokeza ni kulazimika kwa vilabu ya EpL kulipa fedha nyingi zaidi katika usajili kama ambavyo Dr Babatunde Buraimo, mhadhiri wa masuala ya uchumi wa michezo kutoka Chuo Kikuu cha Liverpool, anavyoelezea. “Vilabu vitakuwa na vikwazo katika kusajili wachezaji wenye kaliba ya juu kutoka kwenye mataifa mengine ya ulaya, na matokeo yake kutokuwepo kwa machaguo mengi kutapandisha thamani zaidi ya wachezaji.”
Kushuka Thamani kwa Paundi na Soko la Usajili
Mapema asubuhi ya leo paundi ya Uingereza imeshuka kwa kiasi cha zaidi ya asilimia 10, hivyo hali ikiendelea hivi itamaanisha vilabu vya UK itabidi vilipe zaidi katika usajili wa wachezaji kutokana na kushuka thamani kwa fedha yao.
Tusahau kuwaona Akina Fabregas wapya EPL
Sheria za sasa za UK zinakataza kwa vilabu kusajili mchezaji ambaye sio raia wa nchi za EU ambaye ana umri chini ya miaka 18. Kwa maana hiyo kujiondoa kwa UK ndani ya EU kutaondoa ile ruhusa za vilabu kuwasajili wachezaji walio chini ya umri unaoruhusiwa ambao sio raia wa Uingereza.
Arsenal ilimsajili Fabregas akiwa na miaka 16, Man United iliwasajili akina Pogba, Januzaj, Mensah wakiwa chini ya miaka 18, lakini iliwezekana kutokana na kwamba wakati huo UK ilikuwa mmoja wa wanachama wa EU na wachezaji wote wanatoka ndani ya Umoja huo wa ulaya.
Breaking News: Orodha Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Tano Na Vyuo Vya Ufundi Kwa Mwaka 2016 Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Ijumaa June 24, 2016 Bofya hapa
Habari zilizopo katika Magazeti ya Leo Ijumaa June 24, 2016 Bofya hapa
Magufuli: Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Pumzika Kwa Amani, Wewe upo Salama, Usisikilize kelele za Nje Bofya hapa
Vibonzo Katuni tano bora zaidi leo Ijumaa June 24, 2016 Bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
Vibonzo Katuni tano bora zaidi leo Ijumaa June 24, 2016 Bofya hapa
Like page yetu ya facebook upate habari kwa urahisi na haraka zaidi BOFYA HAPA
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA