KIGOGO TFF ATUA ALGERIA KUIONGEZEA NGUVU YANGA

Pluijm akiongea na Lufano (katikati) mara baada ya kuwasili, kulia ni mwanachama wa klabu hiyo Soud Tall.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Vedastus Lufano amewasili muda huu mjini Bejaia akiuongezea nguvu msafara wa Yanga kuelekea mchezo wa kesho.

Lufano ambaye sasa anakuwa mkuu wa msafara ametua Bejaia mji ambao mchezo wa Yanga wakikutana na Mo Bejaia utafanyika na kwenda moja kwa moja mpaka hoteli ya Raya ambayo Yanga imeweka kambi na kulakiwa na kocha wa timu hiyo Hans Pluijm.

Kigogo huyo ameongozana na mwanachama na komandoo mkongwe wa Yanga Soud Tall na kufanya kikao kifupi na kiongozi wa msafara wa Yanga ndani ya timu hiyo Mohamed Nyenge.Mohamed Nyenge akimlaki Soud kwa furaha

“Nimekuja kuiwakilisha TFF ilikuwa nije na timu lakini kama mnavyojua Yanga wakati wanakuja huku hawakutokea Tanzania walikuwa wanatoka Uturuki kwa hiyo ndiyo sababu ya wao kutangulia,” amesema Lufano.

“Nimefurahi kuona kila kitu kipo sawa nimekutana na kocha amenithibitishia kwamba vijana wako sawa kuelekea mechi ya kesho lakini pia hata kiongozi wa Yanga Mohamed Nyenge amenihakikishia kila kitu kipo sawa sasa naungana nao kuongeza nguvu.
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top