JESUS CORONA AIOKOA MEXICO MIKONONI MWA VENEZUELA


Mexico
Jesus “Tecatito” Corona na Jose Manuel Velazquez walipachika mabao kwenye bonge la game kati ya Mexico na Venezuela mchezo uliomalizika kwa sare ya

kufungana bao 1-1 huku Mexico wakitwaa uongozi wa Kundi C.

Haya ni mambo matatu muhimu yaliyojiri wakati Mexico ikifanikiwa kufuzu kwenda kwenye hatua ya nane bora kwenye michuano ya Copa America Centenario.

Jose Manuel Velazquez alianza kuifungia Venezuela bao la kuongoza lakini Mexico walisawazisha bao hilo kupitia kwa Jesus “Tecatito” Corona dakika 10 kabla ya mechi kumalizika na kuambulia sare ya goli 1-1 kwenye mchezo wa mwisho wa Kundi C ulioshuhudiwa na mashabiki 67,319 kwenye dimba la NRG Stadium huko Houston.

Matokeo hayo yameifanya Mexico kumaliza wakiwa vinara wa kundi C kwa pointi saba sawa na Venezuela lakini wakikaa kileleni mwa kundi kwa tofauti ya magoli na sasa wametengeneza rekodi ya kutopoteza kwenye mechi 22 za mashindano yote ikiwa ni rekodi mpya kwenye timu hiyo ya taifa.

Mexico itacheza dhidi ya Chile au Panama huko Calif, Santa Clara siku ya Jumamosi June 18 wakati Venezuela wanauwezekano mkubwa wa kukutana na Argentina huko Foxborough siku hiyohiyo ya Jumamosi.

Kocha wa Mexico Juan Carlos Osorioalifanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chake kwa kuwapumzisha wachezaji wake tisa wa kikosi cha kwanza wakati wa mchezo huo wa mwisho wa Kundi C huku kocha wa Venezuela Rafael Dudamel yeye akipumzisha nyota wake wanne kutoka kwenye kikosi cha kwanza kilichoichapa Uruguay kwa bao 1-0 kwasababu timu zote tayari zilishafuzu kwa hatua ya robo fainali.

Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top