Moja ya stori zilizowashika wengi Copa America hii ni ile ya Messi kutafuta kombe lake la kwanza akichezea timu yake ya Taifa. Messi alifika karibu sana kufikisha lengo hili kwenye kombe la Dunia la mwaka 2014, na akajaribu tena kwenye Copa America ya mwaka 2015 bila mafanikio. Je mwaka 2016 utakuwa wa kwake?
Lakini kuna mtu mmoja ambaye yeye amekuwa akisubiri kufanikisha hili analotafuta Messi hata kushinda Messi mweneyewe, huyu ni Javier Mascherano. Hakika kwenye hii timu ya Argentina hakuna anayestahili ushindi kama Javier Mascherano.
‘Bosi mdogo’ kama anavyojulikana ameichezea timu yake ya taifa kwa miaka 13. Alicheza mechi yake ya kwanza kwenye timu yake ya taifa mwaka 2003 kabla hata ya kucheza mechi hata moja kwa ajili ya klabu yake River Plate. Lakini hakika Argentina waliona vya kutosha alipokuwa anachezea timu yao ya U-20 na wakatambua kwamba kwa Javier Mascherano walikuwa wamepata mchezaji wa muda mrefu.
Mpaka Copa America ya mwaka 2004 nchini Peru ilipofika hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa anaweza kufikiria timu ya Argentina bila Javier Mascherano. Na ilionekana kwamba basi Mascherano akiwa na miaka 20 tu ataonja ladha ya Ubingwa na timu yake ya taifa mwaka huo. Kwenye fainali ya Copa America hiyo alimkaba vizuri sana namba 10 wa Brazil kwa wakati huo Alex kitu ambacho kilirahisisha kazi ya Argentina kwenye mechi hiyo.
Argentina walikuwa wanaongoza 2-1 mpaka dakika za mwisho za mechi, ila walipigwa ngumi ya tumbo pale Adriano alipofunga goli la ajabu na shuti la mwisho la mechi hiyo .Argentina walifungwa kwenye penati.
Twende mbele miaka mitatu baadaye na Argentina walijikuta kwenye hali ile ile kama ilivyokuwa Peru. Argentina walifikia kilele kipya kwenye michuano hii kwani timu yao ilikuwa na fundi Juan Roman Riquelme ambaye alikuwa akicontroo game na Messi ambaye alikuwa akifanya mambo ya ajabu kama ilivyokuwa kawaida yake.
Argentina walitamba sana kwenye mechi kadhaa kwenye michuano hii kiasi kwamba ata Mascherano mwenyenyewe aliamua kushambulia mara kadhaa na akaweza kujipatia magoli mawili kwenye mechi mbili mfululizo.
Lakini licha ya hayo yote kwa mara nyingine tena Brazil waliwashtukiza Argentina na kuwafunga 3-0 kwenye fainali kwa kutumia mpira wa Counter Attack.
Hii yote ina maanisha kwamba Mascherano amecheza fainali nne na timu yake ya taifa na amefungwa mara zote hizo na kiukweli nafasi zinamuishia. Hivi sasa ana miaka 32 na kombe la Dunia la mwaka 2018 nchini Russia bila shaka litakuwa la mwisho kwake. Wakina Messi, Aguero, Di Maria wanaweza kuendelea hata zaidi ya hapo ila hakika Mascherano yuko karibu zaidi ya mwisho wa barabara.
Kwa sasa hivi anacheza mpira bora zaidi kuliko kipindi kingine chochote kile katika maisha yake. Mchezaji mwenzake kwenye klabu ya Barcelona Dani Alves alisema mwaka jana kwamba yeye anahisi kuwa Mascherano ndiye mchezaji bora zaidi ambaye hapati sifa anazostahili. Nusu fainali ya Jumanne dhidi ya Marekani ilionesha jambo hili.
Watu wengi wanamfikiria Mascherano kuwa ni mchezaji ambaye ni mbabe, mwenye nguvu, anapenda kucheza rafu na ambaye atafanya chcochote kushinda. Japo ni kweli ila Mascherano ana vitu vingine pia. Hakika Pep Guardiola asingemchukua Mascherano kucheza kama beki wake wa kati kwenye timu yake kama asingeamini uwezo wa Mascherano kucheza mpira.
Namba 14 huyu wa Argentina ana uwezo wa kupanga timu yake akiwa nyuma na pia ana uwezo mkubwa wa kusoma jinsi mchezo unavyoenda, huwa anaona hatari mapema sana na anaizima kwa haraka. Hii ndiyo sababu kwanini timu ya Marekani ilishindwa kupiga shuti hata moja golini kwenye Nusu fainali yao dhidi ya Argentina.
Kila ambapo mshambuliaji wa Marekani Clint Dempsey aliposhika mpira alijikuta akipumuliwa na Mascherano nyuma yake.
Hakufanya kosa lolote siku ya Jumanne, mara chache ambapo Mascherano hufanya kosa basi hapo ndipo udhaifu wa timu ya Argentina unapoonekana na hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye mechi ya Robo fainali dhidi ya Venezuela. Kwenye mechi hiyo kosa la Mascherano moja tu liliwapa nguvu timu ya Venezuela na ikawalazimisha Argentina kukaba mashambulizi ya Venezuela kwa kipindi cha dakika 15.
Kosa la Mascherano moja lilileta mtetemko kwenye safu ya ulinzi ya Argentina lakini mwishowe waliweza kushinda basi Mascherano hana budi kucheza bila kosa kama ilivyokuwa kawaida yake kwa mara nyingine tena Jumapili ili aweze kuishindia nchi yake kombe kwa mara ya kwanza.
HABARI KUU LEO BOFYA HAPA