Euro2016: Leo mechi tatu zachezwa

Hii leo kuna mechi tatu katika kinyanganyiro cha mataifa bingwa barani Ulaya. Mechi ya kwanza ni ya kundi la D kati ya Uturuki na Croatia ambayo itachezwa mjini Paris.

Katika kundi la C, Ireland Kaskazini ambayo ilifuzu kwa kombe hilo kwa mara ya kwanza kabisa, watacheza mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Poland katika mji wa Nice.

Ujerumani walioshinda kombe hilo mara ya mwisho miaka 20 iliyopita, itapambana na Ukrain karibu na mji wa Lille.
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top