Breaking news:Jeshi la polisi lawasambaratisha wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma

Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma limewasambaratisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanachama wa Chadema ( Chadema Students Organization -CHASO ) waliokuwa wakishiriki hafla ya mahafali katika Ukumbi wa
African Dreams ulipo Area D mjini Dodoma.

Katika hafla hiyo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambapo baadhi ya wanafunzi wamekamatwa baada ya kuwambiwa watawanyike na kurudi majumbani kwao. 

Polisi wamesema mikusanyiko yote ya kisiasa ilishapigwa marufuku, hivyo hata mahafali hiyo ilikuwa batili



HABARI KUU LEO BOFYA HAPA
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top