Maandamano Pakistan
Maafisa wa polisi katika mji wa Pakistan wa Lahore wamemkamata mwanamke anayetuhumiwa kumuua mwanawe wa kike kwa kufanya ndoa
bila ruhusa ya familia.
bila ruhusa ya familia.
Maafisa wa polisi wanasema mwili wa Zeenat Rafiq una ishara za alama za mateso.
''Alifungwa kamba katika kitanda ,kumwagiwa mafuta na kuchomwa''.
Mamaake anatahumiwa kwa kumchukua kutoka kwa wakweze.
Ni kisa cha tatu katika kipindi cha mwezi mmoja nchini Pakistan ambapo mashambulio ya wanawake wanaokiuka sheria za kihafidhina kuhusu mapenzi na ndoa hufanyika.Image captionMaria Sadaqat
Wiki iliopita mwalimu Maria Sadaqat,alichomwa katika eneo la Murree karibu na mji wa Islamabad kwa kukataa kuolewa.
Alifariki kutokana na majeraha.