Wazazi waficha watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa .


Katika kipindi cha wiki tatu hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha upasuaji kwa kushirikiana na Taasisi ya GSM wamefanikiwa kutoa huduma ya <endelee bofya kichwa cha habari hii juu>matibabu kwa watoto zaidi ya 90 wenye vichwa vikubwa na mgongowazi katika mikoa 5 ya Tanzania bara.

Akiongea na channel ten katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa marogoro daktari bingwa wa magojwa hayo, Osman Kuloloma ,amesema ameshangazwa na idadi ndogo ya wazazi kuwaleta watoto wao kupata matibabu hayo wakati takwimu zinaonyesha kuwa kuna wagongwa wenye matatizo ya vichwa vikubwa na migongo wazi zaidi ya 4000.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi walijitokeza kupata huduma hiyo ya matibabu ya vichwa vikubwa na migongo wazi wamesema kuwa tatizo hilo limekuwa likiwatesa watoto na kuwasababishia kuugua mara kwa mara huku wakiwataka wazazi wenzao kutowaficha watoto wao kwani ugonjwa huo unatibika.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top