Waziri mkuu mpya wa Guinea Bissau
Mawaziri kadhaa waliofutwa kazi nchini Guinea Bissau wiki mbili zilizopita wamekataa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>kung'atuka mamlakani.
Waziri mkuu mpya, Baciro Dja, aliapishwa hapo jana, japo baraza la mawaziri la sasa limekataa kumtambua.
Wanasema angefaa kuteuliwa na chama tawala cha ( PAIGC) na sio rais Jose Mario Vaz.
Uteuzi huo ulisababisha maandamano makubwa siku ya Alhamis.
Tangu mwaka 1974, hakuna kiongozi yeyote wa kuchaguliwa wa taifa hilo, ambaye ametumikia muhula wake kamili.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)