Suleiman Mbuthia ni mmoja wa waliatikana bila hatia
Washukiwa watano walioondolewa makosa ya kuhusika kwenye mashambulio ya mabomu ya <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>mwaka 2010 mjini Kampala, Uganda wamekamatwa tena.
Mawakili wa watano hao wameambia wanahabari kwamba washukiwa hao wamekamatwa na kupelekwa nje ya Kampala.
Gazeti la serikali ya New Vision limeripoti kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ameambia mahakama watano hao walikamatwa kabla ya kufikishwa gereza la Luzira.
Hii ni baada ya wakili wa washtakiwa kulalamikia mahakama kwamba washukiwa waliokuwa wameachiliwa huru walikuwa wametoweka.
Waliopatikana bila hatia ni Abubakari Batemyetto, Omar Awadh Omar, Yahya Suleiman Mbuthia, Mohamed Hamid Suleiman na Dkt Ismael Kalule.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)