Uwekezaji Kwenye Rasilimali Watu Sekta ya Anga

Wakati biashara kwenye sekta ya anga nchini inakuwa kwa kasi, uzalishaji wa rasilimali watu kukidhi uhitaji wa<endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
sekta hiyo hapa nchini ni mdogo hali inayolazimu vitengo vingi kuhudumiwa na wafanyakazi wa kigeni.

Aidha takwimu zinaonyesha kuwa Usafiri wa anga nchini unakuwa kwa asilimia saba kwa mwaka, huku wastani wa abiria kwenye viwanja nchi kwa mwaka ukiwa milioni 5.6.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Anga nchini Mhandisi George Sambali ameyasema hayo wakati wa mahafali ya wahitimu 70 wa kozi mbalimbali za huduma za anga kupitia chuo cha Regional Aviation kilichopo uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Amesema usafiri wa anga umeachwa nyuma kama moja ya eneo la kukuza uchumi wa nchi, hususan kwenye eneo la rasilimali watu, hali inayosababisha shughuli nyingi za sekta ya anga kufanywa na wageni.

Wakati takwimu zinaonyesha Tanzania inajumla ya mashirika ya ndege thelathini yanayotoa huduma zake hapa nchini, na ndege binafsi mia moja, asilimia kubwa ya ndege hizo zinarushwa na wageni, kutokana na tanzania kutokuwa na watalaamu wake, kulikochangiwa kwa kiasi kikubwa na uwekezaji mdogo kwenye rasilimali watu kwenye sekta ya anga.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top