Ujumbe wa kuwepo moshi ndani ya ndege ulipokelewa

Ndege ya EgyptAir ilikuwa na watu 66.

Wachunguzi nchini Ufaransa wamethibitisha ripoti kuwa ndege ya EgyptAir ilituma ujumbe kuwa moshi ulikuwa kwenye ndege hiyo muda mfupi kabla ianguke katika bahari ya <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>Mediterrania.

Shirika la usalama wa safari za ndege linasema kuwa ujumbe huo unamaanisha kuanza kwa moto.

Ujumbe huo ulipokelewa muda mfupi kabla ya ndege hiyo aina ya Airbus A320 kutoweka kutoka kwa mitambo ya radar siku ya Alhamisi.Familia za waathiriwa wa ajali ya ndege.

Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka mjini Paris, Ufaransa na jumla ya watu 66.

Mwandishi wa BBC wa maswala ya Usalama anasema kuwa ajali hiyo huenda ikawa ni ya kawaida au ilisababishwa na mlipuko . Hata hivyo alisema uhakiki hauwezi kujulikana kwa sasa hadi chombo maalumu cha kunasa mawasiliano kwenye ndege kitakapopatikana na kuchunguzwa.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top