Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Jeshi Lupembe, ameanza upya uhakiki wa watumishi wote walio chini ya <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>halmashauri hiyo wapatao 2,427.
Uhakiki huo ambao tayari umefanyika kwenye kata 12 kati ya 21 za manispaa hiyo, umetokana na kubaini uwepo wa watumishi hewa 19 katika uhakiki wa awali ulioagizwa na Rais John Magufuli na kuwezesha kuokoa Sh milioni 33.5.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa watumishi hewa 19 waliobainika awali, tayari wahusika wameandikiwa barua za kurejesha fedha zote kabla ya Mei 30, mwaka huu na baadhi yao wameanza kulipa.
Lupembe alisema ameona ni jambo la busara kufanya uhakiki wa watumishi wote walio chini ya halmashauri hiyo, kwa lengo la kujiridhisha kama watumishi wote wana nyaraka sahihi za ajira, ikiwa ni pamoja na kubaini ambao walipaswa kupandishwa vyeo lakini bado.
Alisema hadi kufikia Mei 16 tayari watumishi 907 walikuwa wamehakikiwa na matarajio ni kuhakiki watumishi wote 2,427.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)