TFF yagomea mamilioni ya Rais Kagame wa Rwanda kupitia nchini

Rais wa Rwanda, Paul Kagame kupitia michuano ya CECAFA katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kila mwaka anatoa kitita kikubwa cha pesa kwa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>ajili ya michuano hiyo yenye historia ambayo hadi sasa ina ukubwa wa miaka zaidi ya 42. Kwani anamwaga fedha zaidi ya dola 60,000 (Sh milioni 120)

Kila msimu wa michuano hiyo ambayo Tanzania kupitia klabu zake imekuwa ikishiriki na hata kunyakua taji hilo mara kwa mara, lakini kwa hatua ya TFF kuyakacha mashindano haya ni kama kumgomea Kagame na mamilioni yake.

Tayari leo Mei 26.2016, Shirikisho hilo la Soka nchini TFF, kupitia kwa taarifa yake kwa vyombo vya habari mchana huu zimeeleza kuwa, hawataandaa michuano hiyo ya kombe la Kagame kutokana na kubanwa na michuamo mbalimbali ya Kimataifa.

Taarifa ya TFF imesema “Shirikisho a Soka Tanzana (TFF), limetangaza kutoandaa michuano ya kuwania Kombe la timu za nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), maarufu kama Kombe la Kagame kwa mwaka 2016 kama ilivyopendekezwa”

Sababu za TFF ya kutoandaa fainali hizo ni kwa kubanwa na ratiba ya michuano ya kitaifa na kimataifa. Awali mkutano mkuu wa CECAFA, uliamua Zanzibar iwe mwenyeji wa michuano ya Kagame. Baadae kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao ilionekana Zanzibar hawataweza kufanya.

Baada ya hapo TFF ilianza kuangalia uwezekano wa mashindano haya kwa kuwashirikisha mabingwa wa 2015/16 ambao ni Yanga.

Kutokana na ratiba ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), kipindi ch Juni hadi Agosti, 2016 Yanga watakuwa na kwenye michuano ya CAF hatua ya makundi hivyo ushiriki wao CECAFA utakuwa mgumu ilihali michuano ya CECAFA imepangwa kufanyika Juni na Julai, mwaka huu.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top