Taliban wamteua kiongozi mpya Afghanistan

Mullah Mansour aliuawa Jumamosi

Kundi la wapiganaji wa Taliban nchini Afghanistan limemteua kiongozi mpya baada ya <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>kuuawa kwa Mullah Mansour.

Bw Mawlawi Haibatullah Akhundzada ndiye kiongozi mpya.

Manaibu wake watakuwa Sirajuddin Haqqani, ambaye mtandao wake umedaiwa kutekeleza mashambulio mengi ya mabomu Kabul, na Mohammad Yaqoob, mwanawe mwanzilishi wa Taliban, Mullah Omar.

Mansour aliuawa katika mkoa wa Balochistan nchini Pakistan kwenye shambulio lililotekelezwa na ndege za Marekani zisizokuwa na rubani.

Rais wa Marekani Barack Obama Jumatatu alithibitisha kifo cha Mansour Jumatatu.

Pentagon ilisema Mansour amekuwa akipanga mashambulio dhidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.
Wapiganaji wa Taliban wamekuwa wakitekeleza mashambulio Afghanistan na Pakistan

Jumanne, waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan Chaudhry Nisar Ali Khan aliambia wanahabari kwamba mwili wa Mansour ulipatikana karibu na mpaka wan chi hiyo na Pakistan.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top