Serikali yaombwa kuwatambua wanaobadili taka kuwa bidhaa

Balozi wa kujitolea wa mazingira, Omary Kombe ameiomba Serikali kuwatambua watu wanaobadilisha taka kuwa bidhaa kwa kuendeleza taaluma hiyo ili kuinua uchumi na<endelea bofya kichwa cha habari hii juu>

kuondokana na tatizo la uchafu nchini.

Akiongea na waandishi wa habari Mei 18, 2016 jijini Dar es Salaam, Kombe alisema kwamba kwa kuwatambua watu hao, tatizo la taka litakwisha kwa kiwango kikubwa nchini hasa katika jiji la Dar es Salaam.

“Wapo watu ambao mara nyingi tunawaona kwenye maonyesho mbalimbali kama vile sabasaba ambao wanauwezo wa kubadili taka kuwa bidhaa za majumbani kwa mfano, mkaa, mapambo na bidhaa nyingine, ni vizuri Serikali ikawatumia watu hao kuondokana na tatizo la taka nchini,” alisema Kombe.

Aliongeza kwamba mazingira bado ni machafu licha ya serikali ya awamu ya tano kuweka mkazo katika suala zima la usafi kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu.

Kombe alisema kwamba, tatizo hilo la uchafu litatatuliwa kama watu wenye uwezo wa kubadilisha taka kuwa bidhaa watatambuliwa na kufanya kazi hiyo kuwa rasmi.

Aidha alisema kuwa, kwa kubadilisha taka kuwa bidhaa kutapunguza kiwango cha taka nchini, kuongeza ajira pamoja na kuipunguzia Serikali mzigo wa kutenga maeneo kwa ajili ya kuhifadhia taka kila mara.

Usafi ni kauli mbiu ambayo imeshika kasi awamu hii ya tano ambapo katika sherehe za Uhuru (Tisa Desemba) Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliwataka watanzania wote kushiriki usafi maeneo yanayowazunguka na vituo vya jamii kama hospitali, zahanati na vituo vya afya.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top