Serikali imeeleza mkakati wa kuzirudisha shule 33 maarufu katika ubora wake ili <endela bofyqa kichwa cha habari hii juu>ziweze kufanya vizuri kama ilivyokuwa zamani.
Mkakati huo ulielezwa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alipokuwa akiwasilisha hotuba ya bajeti yake bungeni.
Alisema shule hizo zilipokuwa nzuri zikitoa elimu bora, zilizalisha vipaji vingi, akiwamo yeye aliyesoma katika mojawapo.Alisema katika awamu ya kwanza, shule 33 zitakarabatiwa.
Alizitaja shule hizo kuwa ni Ihungo, Ilboru, Kilakala, Mwenge, Msalato, Mzumbe, Ngaza, Pugu, Same, Tabora Boys na Tabora Girls.
Nyingine ni Azania, Jangwani, Kantalamba, Mpwapwa, Tosamaganga, Malangali, Milambo, Nangwa, Kibiti, Minaki, Ifakara, Songea Boys, Ndanda, Kigoma, Kibaha na shule za ufundi za Bwiru Boys, Ifunda, Iyunga, Moshi, Mtwara, Musoma na Tanga.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)