Rio Olimpiki
Hadi wanariadha 31 kutoka michezo sita tofauti huenda wakapigwa marufuku kutoshiriki katika michezo ya Olimpiki, kulingana na maafisa wa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>mashindano hayo.
Tangazo hilo linajiri baada ya kamati ya kimataifa ya Olimpiki kukagua violezi kutoka kwa michezo ya Olympiki ya Beijing 2008.
Kamati hiyo ya IOC imesema kuwa vipimo hivyo vilikaguliwa kwa kutumia teknolojia mpya ya kisayansi .
Pia imebaini kwamba inangojea matokeo vipimo vyengine 250 kutoka kwa michezo ya Olympiki ya mwaka 2012 mjini London.
''Mikakati yote hii inalenga kuwazuia wanaodanganya kutoshinda'',rais wa wa IOC Thomas Bach alisema.Olimpiki
''Matokeo hayo yanaonyesha kwa mara nyengine kwamba wale wanaotumia dawa za kusisimua misuli hawana pa kujificha''.
''Tunaweka violezo kwa miaka 10 ili wadanganyifu wajue kwamba hatutachoka''.
''Kwa kuwazuia wale waliodanganya kushiriki mjini Rio,tunaonyesha kwa mara nyengine kwamba tunaweka juhudi za kulinda maadili ya mashindano haya ya Olympiki''.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)