Baada ya kocha wa Uingereza, Roy Hodgson kumuamini mchezaji kinda wa Manchester United, Marcus Rashford na kumweka katika kikosi cha timu ya<endelea bofya kichwa cha habari hii juu> taifa, mchezaji huyo ameanza vizuri katika michezo ake ya timu ya taifa kwa kuisaidia kupata ushindi wa goli 2-1 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Australia.
Rashford ambaye ana miaka 18 aliifungulia milango Uingereza katika dakika ya 3 baada ya kuunganisha mpira mrefu na kuingia moja kwa moja golini na baadae dk. 55 nahodha wa timu hiyo, Wayne Rooney akaiongezea Uingereza goli la pili baada ya kupiga shuti kali lililomshinda nguvu goli kipa wa Australia, Mat Ryan.
Australia baadae ilipata goli la kufutia machozi baada ya mchezaji wa Uingereza, Eric Dier kujifunga goli katika dakika ya 75 na mpaka mchezo huo unamalizika Uingereza ikaibuka na ushindi wa goli 2-1.
Kwa goli hilo ambalo alifunga Rashford limemweka katika mazingira mazuri kwa kuanza vyema kuichezea timu ya taifa ya Uingereza jambo linaloweza kumsaidia kupata nafasi katika michuano ya Euro ambayo yanataraji kuanza mwezi ujao nchini Ufaransa.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)