Rais Obama atembelea mji wa Hiroshima

Obama akiwa Japan
Rais Barrack Obama amekuwa rais wa kwanza aliye mamlakani nchini Marekani kutembelea mji wa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>Hiroshima tangu shambulio la nuklia wakati wa vita vya pili vya dunia.

Obama amesema kuwa kumbukumbu za tarehe 6 mwezi Agosti 1945 hazifai kusahaulika,lakini hakuomba msamaha wa shambulio hilo la Marekani ikiwa ni bomu la kwanza la kinyuklia kutumika duniani.Obama akiwasili mjini Hiroshima

Bw Obama alizungumza na baadhi ya walionusurika na katika hotuba yake akayataka mataifa kujiendeleza bila silaha za kinuklia.

Takriban watu 140,000 walifariki mjini Hiroshima na wengine 74,000 siku mbili baadaye katika bomu la pili katika mji wa Nagasaki.Obama akiweka shada la maua katika makavazi ya kumbukumbu ya Hiroshima

Bw Obama alitembelea makavazi ya Heroshima kabla ya kuelekea katika eneo la kuhifadhi kumbukumbu za shambulio hilo,akiandamana na waziri mkuu Shinzo Abe.Wote wawili walisimama mbele ya mwanga wa milele.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top