Picha mpya za mabaki ya EgyptAir zatolewa

Jeshi la misri limetoa picha za vifaa vilivyopatatikana wakati wa shughuli ya kutafuta ndege iliyopotea ya EgyptAir katika bahari ya Mediterranean.

Kati ya picha zilizowekwa ni pamoja na <endelea bofya kichwa cha habari hii juu >jaketi za kuokoa maisha, sehemu za viti, na vifaa vingine vyenye nembo ya EgyptAir.

Ndege hiyo ilikuwa ikitokea mjini Paris nchini Ufaransa ikiwa na watu 66, wakati ilitoweka kutoka kwa mitambo ya radar siku ya Alhamisi.

Wachunguzi nchini Ufaransa wamethibitisha ripoti kuwa ndege hiyo ilituma ujumbe kuwa moshi ulikuwa kwenye ndege muda mfupi kabla itoweke.

Lakini hata hivyo wanasema kuwa chanzo cha kuanguka kwa ndege bado hakijulikani.

Shughuli hiyo ya kutafuta pia imepata sememu za wanadamu na mizigo.

Sehemu kubwa ya ndege hiyo na visanduku viwili vya kunasa mawasiliano ya ndege havijapatikana.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top