Muhtasari: Habari kuu leo Ijumaa May 27, 2016 kutoka BBC

Miongoni wa habari nyingine kuu leo, viongozi wa G7 wameahidi kuimarisha uchumi duniani, Trump amefurahia kupata wajumbe wa kutosha na viini maradhi sugu visivyosikia dawa vimegunduliwa Marekani.
1. Viongozi wa G7 wajitolea kuimarisha uchumi
Viongozi wa mataifa saba yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi duniani maarufu kama G7, wanasema uimarishaji wa<Endelea bofya kichwa cha habari hii juu> uchumi duniani ni swala linalofaa kupewa kipau mbele.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari baada ya mkutano wa viongozi hao nchini Japan, G7 imeahidi kuhakikisha kuwa masoko ya kimataifa yamesalia kuwa wazi, na kuzuia mbinu zozote za ulinzi wa soko, dhidi ya ushindani wa masoko ya nje.
2. Obama rais wa kwanza Mmarekani kuzuru Hiroshima
Rais wa marekani Barrack obama atakuwa rais wa kwanaza wa taifa hilo kuzuru mji wa Hiroshima nchini Japan hivi leo, eneo la mlipuko wa bomu la kwanza la atomiki duniani.

Rais Obama anatarajiwa kuweka shada la maua katika eneo hilo, kuwakumbuka watu 140,000 walioaga dunia, kutokana na shambulizi hilo lililotekelezwa na marekani.
3. Wafuasi wavamia ikulu Guinea-BissauBBC WORLD SERVICE

Wafuasi wa chama tawala nchini Guinea-Bissau wamevamia ikulu ya rais, wakipinga uteuzi wa waziri mkuu mpya.

Zaidi ya watu 100 waliandamana na kuchoma moto tairi huku wakirusha mawe.
4. Trump afurahia kupata wajumbe wa kutoshaAFP

Donald Trump ameelezea furaha yake kwa kupata uungwaji mkono na wajumbe wa kutosha kutoka chama chake cha Republican.

Hiyo inamhakikishia uteuzi wa chama hicho kuwania urais katika uchaguzi mkuu Novemba mwaka huu.

Anatarajiwa kumenyana na Hillary Clinton, ambaye amemtaja Trump kuwa, mtu asiyetabirika, anayeweza kusababisha madhara makubwa.
5. Maafisa wagundua bakteria sugu Marekani.

Maafisa wa afya nchini marekani wanasema bakteria hatari inayostahimili athari za antibiotiki zote zinazojulikana duniani imegunduliwa nchini humo kwa mara ya kwanza.

Hii ni baada ya mwanamke mmoja kupatikana na bakteria aina ya E-Coli, iliyo na kinga dhidi ya antibiotiki iliyo na nguvu zaidi ya Colistin.
6. Uingereza kutuma manowari nyingine LibyaI
Uingereza inasema itatuma manowari nyingine nchini Lybia, kusaidia kutoa mafunzo kwa walinzi wa baharini nchini humo.

Hii ni katika juhudi za kusitisha ulanguzi wa binadamu kupitia bahari ya Mediterranean.

Aidha maafisa hao wanasema wanatafuta kibali cha Umoja wa Mataifa cha kuwawezesha kukamata meli zote zinazosafrisha silaha kimagendo kwa kundi la Islamic State.
7. Google waishinda Oracle kesi ya JavaJAVA LOGO

Kampuni ya teknolojia ya google imepata ushindi mkubwa katika mahakama moja nchini Marekani. Jopo la waamuzi limeamua kuwa Google ina haki ya kutumia programu ya Java katika vifaa vyake vinavyotumia Android bila malipo yoyote.

Kampuni ya Oracle inayomiliki Java, iliifikisha Google mahakamani kwa madai kuwa ilikiuka hakimiliki yake kwa kutumia programu hiyo.
8. Serikali yapewa mamlaka kutwaa ardhi Afrika KusiniREUTERS

Chama tawala cha ANC nchini Afrika kusini kimepongeza kura iliyopigwa na bunge la taifa hilo, ya kuipa serikali mamalaka ya kutwaa ardhi yoyote kwa maslahi ya umma.

ANC inasema sheria hiyo itawapa haki raia wengi wa taifa hilo waliopokonywa mashamba yao.
9. Raia wasimulia madhila ndani ya FallujahAP
Raia wachache ambao wamejinasua kutoka mji uliozingirwa wa Fallujah nchini Iraq wanasema kuwa mji huo unakumbwa na matatizo chungu nzima ya kibinadam.

Zaidi ya watu 50,000 wamekwama mjini humo, wakati ambapo vikosi vya taifa hilo vinajitayarisha kufanya uvamizi wa kuukomboa mikononi mwa wapiganaji wa Islamic state.

Familia kadha zimeelezea hofu yao kuwa huenda zikaangamia kutokana na njaa, endapo hawatookolewa.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top