Muhtasari: Habari kuu leo Alhamisi, kutoka BBC Swahili

Miongoni mwa habari kuu leo, majimbo 11 yameishtaki serikali ya Rais Obama nchini Marekani na polisi Kenya wanasaka washukiwa wa Islamic State.

1. Majimbo 11 Marekani yashtaki serikali ya Obama
Image copyrightGETTY
Majimbo 11 nchini Marekani yameushtaki utawala wa Rais Barack Obama, kufuatia agizo kuwa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
wanafunzi walioegemea jinsia tofauti na ya kuzaliwa wanafaa kuruhusiwa kuchagua ni vyoo gani watatumia.
Utawala wa nchi hiyo umetishia kufutilia mbali ufadhili kwa shule za serikali, ambazo hazitafuatia magizo hayo. Lakini kesi hiyo iliyowasilishwa katika jimbo la Texas itaituhumu serikali kwa kufanya majaribio makubwa ya kijamii.

2. Utafiti: Kudorora kwa uchumi 2008 kulizidisha vifo

Image copyrightAP
Utafiti mpya unaonyesha kuwa mzozo mkubwa wa kifedha duniani wa mwaka 2008, ulisababisha kupanda kwa kasi vifo vinavyohusiana na maradhi ya saratani, katika mataifa 35 yaliyoendelea duniani.
Kulishuhudiwa vifo 260,000 katika kipindi cha miaka miwili iliyofuata mdororo huo wa kifedha ambavyo vilichangiwa na ukosefu wa kazi, pamoja na upungufu wa matumizi ya fedha za matibabu.
Hata hivyo, katika mataifa yenye mpangilio bora wa matibabu kama vile Uingereza na Uhispania, hakukushuhudiwa ongezeko la vifo.

3. UN yafutilia mbali vikwazo dhidi ya Liberia

Image copyrightGETTY IMAGES
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, limepiga kura kwa kauli moja, kufutilia mbali baadhi ya vikwazo dhidi ya Liberia, katika jitihada za kufuta kabisa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya taifa hilo mnamo mwaka 1992.
Kuna muafaka wa amani ulioafikiwa na Liberia na kupongezwa kwa hatua zake za kutekelezwa upya tangu kumalizika kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, mnamo mwaka 2003.
Umoja wa Mataifa pia unaondoa majeshi yake ya kulinda amani nchini humo.

4. Polisi wakabiliana na walemavu Bolivia

Image copyrightAP
Polisi nchini Bolivia, wamekabiliana vikali na waandamanaji walemavu waliojaribu kufikia ikulu ya Rais kudai kile wanachosema ni manufaa kutoka kwa nchi.
Serikali ya nchi hiyo inasema kuwa polisi walikabiliwa na waandamanaji hao kwa visu na gesi wakitaka kupita kizuizi kilichowekwa na polisi.
Polisi walijibu kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.
Walemavu hao wamekita kambi La Paz kwa mwezi mmoja wakitaka kuongezewa marupurupu yanayopewa walemavu.

5. Polisi Kenya wasaka washukiwa wa Islamic State

Idara ya Polisi nchini Kenya inaendelea na msako wa kusambaratisha mtandao wa kundi la wapiganaji la ISIS, ambalo linataka kukita mizizi yake nchini humo kwa lengo la kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wananchi wasio kuwa na hatia.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na inspekta mkuu wa polisi Nchini Kenya.

6. Mwanamuziki nyota wa Cameroon Anne Nzie afariki

Mwanamuziki mtajika mno nchini Cameroon, Anne Marie Nzie, amefariki akiwa na umri wa miaka 84. Akifahamika kwa sauti mufti mithili ya dhahabu nchini Cameroon, aliboresha mno sauti yake na kuwa dhahabu ya Cameroon.
Image copyrightGETTY
Alivuma sana kwa ngoma yake iliyobobea ya "Liberte" iliyokuwa ikishinikiza kuwepo kwa uhuru zaidi na utawala wa kidemokrasia.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top