Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul makonda ameanzisha mkakati wa kukoa Ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya watumishi wa Serikali baada ya <endelee bofya kichwa cha habari hii juu>kubaini kuwa magari mengi yanatelekezwa na baadae kuuzwa kwa bei chini kwa baadhi ya watumishi kwa madai kuwa ni mabovu yaliyoshindikana kutengenezwa.
Akizungumza wakati wa zoezi la kuondoa magari nane ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa dsm ambayo yanadaiwa kukaa muda mrefu kwa madai kuwa mabovu ambayo yangehitaji fedha nyingi kutengeza Bw,Makonda amesema kuna watumishi wamekuwa sio waadilifu ambao wamekuwa wakitumia mwanya huo kujiuzia magari kwa bei ya kutupa.
Amesema Mafundi Magari kutoka Tegeta wameamua kuchukua magari hayo na kutengeneza Bure ikiwa ni mchango wao katika kuisaidia serikali ya awamu ya tano katika kuwatumikia wananchi.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)