Mourinho athibitishwa meneja mpya Manchester United

Mourinho alifutwa kazi Chelsea Desemba

Jose Mourinho ametangaza rasmi kuwa meneja mpya
wa<endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
klabu ya Manchester United.

Ametia saini mkataba wa miaka mitatu.

Mreno huyo anachukua nafasi ya Mholanzi Louis van Van Gaal, aliyefutwa kazi Jumatatu siku mbili baada ya kushinda Kombe la Dunia.

"José kusema kweli ndiye meneja bora zaidi wa soka kwa sasa," naibu mwenyekiti mtendaji wa United Ed Woodward amesema.

Mourinho, 53, amesema: "Kuwa meneja wa Manchester United ni heshima kubwa sana katika mchezo huu. Ni klabu inayofahamika sana na kuenziwa kote duniani.”

Amesema amekuwa akihisi mvuto wa kutaka kuwa Old Trafford na kwamba daima amekuwa akisikizana na mashabiki wa United.

“Nasubiri kwa hamu kuwa meneja wao na kujivunia uungwaji mkono wao miaka ijayo.

“Kuna hisia fulani na upendo ambao huwezi kupata kutoka kwa klabu nyingine.”

Mourinho amekuwa bila kazi tangu afutwe na klabu ya Chelsea Desemba mwaka jana.

Mourinho ametia saini mkataba baada ya mazungumzo ya siku tatu baina yake, wakala wake Jorge Mendes na maafisa wakuu wa United.

Moja ya mambo ambayo anatarajiwa kuyafanya ni kumchukua mshambuliaji kutoka Sweden Zlatan Ibrahimovic, ambaye walifanya kazi pamoja wakiwa Inter Milan.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top