Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni ya <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za watu wanaotoa rushwa au kupokea rushwa kwaajili ya kuboresha mapambano dhidi ya Rushwa ambapo uzinduzi huo umeambatana pamoja na uzinduzi wa matumizi mapya ya simu ya Dharura ya 113 unayoweza kupiga na kutuma sms za kawaida Uzinduzi huo umefanyika leo katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Tehama TAKUKURU, Neema Mwalyelye akitoa maelekezo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipotembelea kwenye banda la kitengo cha Tehama wakati wa uzinduzi wa kampeni ya LONGA NASI inayomaanisha Sema au ongea na TAKUKURU kwa kutoa Taarifa za watu wanaotoa rushwa au kupokea rushwa iliyofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kamba kuashiria uzinduzi wa gari la matangazo ya Kampeni ya kupambana na Rushwa ya LONGA NASI kwa kupiga namba 113 na kutuma kutuma sms kwenda namba 113 ili kutoa taarifa ya kutoa au kupokea Rushwa kwa TAKUKURU.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)