Makamu Mkuu wa Shule Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumlawiti Mwanafunzi Wake

MAKAMU Mkuu wa Shule ya Sekondari Usevya katika Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele , Makonda Ng’oka “Membele” (34) amefikishwa katika Mahakama ya<endelea bofya kichwa cha habari hii juu> mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake.


Mshtakiwa huyo alifikishwa juzi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Tengwa ambapo alikana shitaka lake na yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kulipa kiasi cha Sh 3,000,000 mahakamani.


Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Gregory Mhangwa alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo katika shule ya sekondari Usevya kati ya Novemba 2015 na Aprili 2016.


Alieleza mahakamani hapo kwamba katika kipindi hicho mshtakiwa alimuingilia mwanafunzi wake huyo kinyume cha maumbile. Hakimu Tengwa aliahirisha shauri hilo hadi Juni 26 , mwaka huu litakapotajwa tena.


Inadaiwa kuwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule hiyo kunafuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano katika shule hiyo kumkataa na kutishia kuandamana kupinga vitendo vyake vya kuwalawiti wanafunzi wake.


Kufuatia msimamo wa wanafunzi hao iliwalazimu Ofisa Elimu mkoa wa Katavi, Everest Hunji na Mkurugenzi Mtendaji Halmashari ya Mpimbwe wilayani Mlele, Evaristo Kiwale kufika shuleni hapo Jumatatu jioni na kuzungumza na wanafunzi hao.


Wanafunzi hao walidai kuwa mwalimu huyo amekuwa akiwalawiti baadhi yao ikiwa ni adhabu mbadala wanapobainika kufanya makosa shuleni hapo. 


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe, Kiwale alisema vitendo vya ushoga havikubaliki na kwamba tayari hatua stahiki zimeshachukuliwa za kumpeleka katika vyombo vya kisheria. 


“Msitaharuki mnapomuona mwalimu huyo mitaani msidhani hajachukuliwa hatua yoyote ile,” alisisitiza.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top