Joaquin "El Chapo" Guzman kuhamishiwa Marekani

Joaquin Guzman, almaarufu El Chapo alikamatwa mwezi Januari.

Mexico imeidhinisha kuhamishiwa Marekani mlangunzi mkuu wa madawa ya <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>kulevya, Joaquin Guzman, almaarufu El Chapo, ili ashtakiwe kwa mauaji na ulanguzi wa madawa ya kulevya.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya imesema kuwa Marekani imehakikishia taifa hilo jirani kuwa Guzman hatahukumiwa kifo katika kesi zinazomkabili.Mawakili wa Guzman wamesema kuwa watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Hivi majuzi Guzman alihamishiwa gereza moja lililoko nchini Mexico hadi lingine lenye ulinzi mkali kwenye mpaka na Marekani.

Mawakili wa Guzman wamesema kuwa watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

El Chapo, aliyesimamia kundi la walanguzi wa madawa ya kulevya lijulikanalo kama Sinaloa alikamatwa Januari, miezi sita baada ya kutoroka kutoka gereza moja la Ulinzi Mkali kwa kuchimba mtaro chini ya ardhi hadi katika seli yake.

Post a Comment

Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright UCHAMBUZI LEO | Modified By Smart WEB
Back To Top Back To Top