Nchini DRC
polisi imesambaratisha mkutano wa upinzani Kinshasa, Mei 26, 2016.
Upinzani mjini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo umefanya maandamano Alhamisi hii kabla ya<Mendelea bofya kichwa cha habari hii juu> kutawanywa na polisi.
Maandamano hayo yalikua yakipinga uamuzi wa Mahakam ya katiba inayomruhusu Joseph Kabila kuongoza nchi hiyo endapo uchaguzi hautafanyika mwaka huu, baada ya muhula wake wa pili kumalizika mwezi Desemba
Maandamano yalianza saa 5:30 Alhamisi hii mchana, saa za mjini Kinshasa. Pamoja na kuchelewa kwa sababu mkutanoulikua umepangwa saa 4:00.
Maandamano yalifanyika kwa haraka. Umati wa watu ulikua umeitikia maandamano hayo, na watu walikua wakiongezeka kila baada ya dakika. Askari polisi walikuwa kandokando ya barabara na walikua hawawasumbui waandamanaji, hata wanajeshi pia.
Martin Fayulu, kiongozi wa chama cha ECIDE, na mgombea urais, ambaye ni mmoja wa viongozi wa vyama vya upinzani walioshiriki maandamano hayo ameeleza kwamba wameamua kuingia mitaani ili kumwambia Bw Kabila kwamba nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
"hakuna mtu atakae kaa milele kwenye kiti cha urais. Katiba iko wazi: anapaswa kuheshimu Katiba kama raia wote wa Congo wanapaswa kuheshimu Katiba. Hilo ni jambo la kwanza. Jambo la piili, kuiambia Mahakama ya Katiba kwamba, inapaswa kuheshimu Katiba, na kuiambia CENI [Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi] kwamba hakuna hoja nyingine lakini kuandaa uchaguzi, kwa sababu Ibara ya 73 inaamuru hivyo. Ni muhimu, uchaguzi wa rais unapaswa kupangwa na kuiitishwa siku 90 mwishoni mwa muhula. Na hatimaye, kuuwambia ulimwengu kwamba tuna mshikamano kwa kile kinachoendelea katika wilaya ya Beni, kwamba sote tunaangalia, na kwamba hakuna serikali yenye uwezo wa kulinda raia wake. Watu wanauawa wilayani Beni. Hizi ni sababu za msingi za maandamano yetu ya leo.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)