Klabu ya Golden State Warriors ilimaliza msimu ikiwa na rekodi ya kushinda michezo 73na kupoteza 9 hivyo kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na klabu ya<endelea bofya kichwa cha habari hii juu>
Chicago Bulls ya kushinda michezo 72-10.Hii ni rekodi ambayo ilichagizwa na mchezaji Stephen Curry ambaye pia alishinda tuzo ya mchezaji bora mwenye thamani kwa kupata kura zote na kuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo katika historia ya NBA.
Chicago Bulls ya kushinda michezo 72-10.Hii ni rekodi ambayo ilichagizwa na mchezaji Stephen Curry ambaye pia alishinda tuzo ya mchezaji bora mwenye thamani kwa kupata kura zote na kuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo katika historia ya NBA.
Warriors walikuwa wakipewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa NBA msimu huu lakini mategemeo hayo almanusura yaingie doa. Wakiwa wamefika katika hatua ya Fainali ya kanda ya Magharibi kwa kuwatoa Portland Trail Blazers walikutana na Oklahoma City ambayo ilikuwa imetoka kuwaondoa San Antonio Spurs ambao walikuwa na rekodi bora ya pili nyuma ya Warriors.
Hata hivyo baada ya michezo minne klabu ya Warriors ilijikuta ikiwa nyuma kwa kufungwa michezo 3 huku ikiwa imeshinda 1 pekee. Hii iliwabidi kutakiwa kushinda michezo 3 iliyosalia ili kuwa mabingwa wa kanda ya Magharibi na ili kuingia katika faibali za NBA. Oklahoma City walitakiwa kushinda mchezo mmoja pekee ili watangazwe mabingwa wa Magharibi na waingie Fainali.
Warriors walishinda michezo miwili mfululizo na kufanya matokeo kuwa 3-3. Hivyo alfajiri ya leo ukapigwa mchezo wa saba ambao ulifanyika nyumbani kwa Warriors katika uwanja wa Oracle Arena. Katika mchezo huo Curry alifunga pointi 36 na kuiongoza Warriors kuibuka na ushindi wa pointi 96-88.
Warriors sasa itakutana na klabu ya Cleveland Cavaliers katika fainali hivyo kufanya marudio ya fainali za msimu uliopita. Warriors imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza tangu mwaka 1981 kuweza kushinda fainali za kanda yoyote huku zikiwa zimefungwa 3-1. Mara ya mwisho ilikuwa Boston Celtics iliyokuwa ikiongozwa na Larry Bird.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)