BUNGE limekanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii na watu wanaodaiwa kuwa ni madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>Misungwi mkoani Mwanza.
Taarifa hiyo inadai kuwa video iliyomuonesha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akijibu swali bungeni Mei 20 mwaka huu, ilihaririwa na kusambazwa na maafisa wa Bunge.
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Bunge kilitoa taarifa ya ufafanuzi kuhusu madai ya kuhaririwa kwa video hiyo, mjini Dodomajana.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa taarifa hizo, si za kweli na zina lengo la kuupotosha umma, kwani ukweli ni kwamba kipindi cha maswali na majibu bungeni, hurushwa moja kwa moja na hupatikana kupitia vituo vyote vya televisheni, vinavyopokea matangazo ya bunge.
Ilisema matangazo hayo, yanaweza pia kurekodiwa na mtu yeyote mwenye uwezo huo popote alipo, kadri anavyoweza kuyapokea matangazo.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)