Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako ameivunja bodi ya Tume ya Vyuo Vikuu na kuwasimamisha kazi viongozi wa <endelea bofya kichwa cha habari hii juu>Tume hiyo, baada ya kubainika kuwadaili wanafunzi 489 wasio na sifa ya kusoma elimu ya chuo kikuu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, ametaja sababu za kuivunja bodi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Dk. Hawadhi Man’genya:
Mbali ya kuivunja bodi ya TCU, Profesa Ndalichako amewasimamisha kazi viongozi wanne wa tume hiyo, kwa niaba ya Rais John Magufuli, aliyetumia madaraka aliyopewa na katiba ya nchi, kupitia ibara ya 36.
Lakini pia waziri huyo wa elimu amewateua watu wawili, ili shuguli za tume ya TCU zisikwame.
Pamoja na mambo mengine, waziri Ndalichako akavitahadharisha vyuo vikuu nchini kuhusiana na kudahili wanafunzi wasio na sifa pamoja na kutolewa mikopo kwa wanafunzi hewa nchini.
Mnamo mwezi februari mwaka huu, ulifanyika ukaguzi na kubainika kuwepo kwa matatizo ya ithibati katika chuo kikuu cha st. Joseph kwenye kampasi zake za Arusha na Songea, na kuamriwa chuo hicho kufungwa na wanafunzi wake kuhamishiwa katika vyuo vikuu vingine.
Post a Comment
Toa maoni tu (kejeli na matusi marufuku)